Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Hussein Ehsani, katika kumbukumbu ya mashahidi iliyofanyika katika Shule ya Azadi, iliyopo katika mji wa Qanawat, mkoani Qom, na kuhudhuriwa na kundi la wanafunzi, walimu pamoja na familia tukufu za mashahidi, aliwasilisha salamu maalumu za Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa familia za mashahidi wa tukio la «Handaki la Nafas» (Tunnel-e Nafas). Aidha, aliwakabidhi familia za mashahidi saba wa Qom waliofariki katika tukio hilo skaf pamoja na zawadi iliyobarikiwa, vilivyotolewa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akitoa salamu za rambirambi kufuatia siku za kumbukumbu ya kuuawa kishahidi Bibi Fatimah Zahraa (as), alisema kuwa kuiga mifano bora ni miongoni mwa mambo yenye mchango mkubwa katika kuelekeza maisha ya mwanadamu na kumsaidia kuchagua njia sahihi.
Alieleza kuwa: “Jamii ya Kiislamu imejaaliwa kuwa na mifano halisi na yenye thamani kubwa ya kuigwa. Hata hivyo, katika kuwatambulisha na kuwaeleza vijana kuhusu mifano hiyo, bado hatujachukua hatua zinazostahili kwa kiwango kinachotakiwa.”
Mkuu huyo wa Kituo cha Huduma za Hawza, akizungumzia mwelekeo wa baadhi ya watu kuvutiwa na mifano ya kimaada, alisisitiza umuhimu wa kuweka mkazo zaidi katika kuwatambulisha vijana mifano halisi na yenye thamani inayopatikana ndani ya jamii ya Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alitoa shukrani kwa juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule pamoja na walimu wake, akibainisha kuwa kufanya kazi katika nyanja ya elimu na malezi ni jukumu gumu linalohitaji moyo wa kujitolea na kufanya kazi kwa ari ya jihadi.
Maoni yako